Maisha

Walemavu walia kusahauliwa sekta ya Viwanda

Tarehe July 25, 2017

Mlemavu wa miguu mkazi wa Jiji la Arusha,

Mlemavu wa miguu mkazi wa Jiji la Arusha akiuza viatu kama alivyokutwa na mpiga wetu.

Walemavu wamedai kuachwa nyuma katika fulsa mbalimbali zinazojitokeza hapa nchini kutokana na hali yao wakati Serikali inaelekea kwenye uchumi wa Viwanda

Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA amesema Sera za kuwashirikisha walemavu kwenye uchumi wa Viwanda bado zinatia shaka hivyo kupelekea wao kuachwa nyuma.

Amesema changamoto nyingine inayowarudisha nyuma walemavu ni  kuwepo mila potofu kwa kuwa hata pale ambapo ulemavu  ulitakiwa kuondolewa  kwa kupelekwa  hospitali  lakini jamii huhusisha na waganga wa kienyeji.

Kwa upande wake  muwasisi wa chama cha walemavu Tanzania Juma bilali alisema rai ya walemavu ni kupatiwa kumiliki ardhi  na kupatiwa elimu bora pamoja na kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

Aliongeza kuwa wao kama Chama cha Walemavu wanakumbushia kutengenezewa mazingira mazuri ya kumiliki Bajaji ambazo kwa sasa  zinaachwa na kuendeshwa na  watu wa kawaida.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni