Maisha

Vifahamu vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017

Tarehe June 9, 2017

DSC04485

Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo vikuu bora zaidi duniani imetangazwa, ambapo chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado kinaongoza.

Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard – pia kutoka Marekani – kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000.

Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.

Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings

  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford
  3. Harvard
  4. California Institute of Technology (Caltech)
  5. Cambridge
  6. Oxford
  7. University College London
  8. Imperial College London
  9. Chicago
  10. ETH Zurich

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni