Maisha

Usithubutu kumpa mimba mwanafunzi, ‘umekwisha’

Tarehe June 7, 2017

Mimba

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakumbusha wanaume wanaomendea wanafunzi kuwa adhabu ya miaka 30 jela iko pale pale.

Akizungumza Lugalo jeshini Jijini Dar es Salaam wakati akizindua na kukabidhi vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayebainika amemkatisha mwanafunzi wa kike masomo kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya ukatili vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka 30 jela.

Katika uzinduzi huo vifaa vya maabara  vya jumla  ya Shilingi Bilioni 16.9 vitatolewa  kwa ajili ya shule 1696 kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uboreshaji wa masomo ya sayansi.

Majaliwa ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha wanakamilisha maabara za shule zote nchini 4587 ambazo bado hazijakamilika ili vifaa hivyo vianze kusaidia wanafunzi kwa haraka na kufikia malengo ya nchi ya kuwa ya uchumi wa kati.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni