Maisha

Ubovu Barabara:Wananchi Vingunguti waiangukia Serikali

Tarehe July 27, 2017

Barabara kutoka maeneo ya barakuda darajani Vingunguti.

Barabara kutoka maeneo ya barakuda darajani Vingunguti.

Wananchi  wa  Vigunguti  wameiomba Serikali  kuboresha   barabara     kutoka  maeneo  ya  Barakuda  Darajani  hadi  maeneo  ya  kwa  tambi  jijini  Dar  es  salaam

Wakizungumza   na  mtandao huu  walikuwa na haya ya kusema,

Hassan   katunda  (34) mkazi  wa  Vingunguti  amesema  Wananchi  wamekuwa wakiteseka   kwa  muda  mwingi  kuhusu  barabara hiyo, hivyo kupelekea  kuchelewa  kazini  kutokana  na  ubovu   wa  barabara

Mwanaidi  Juma  mkazi  wa  Vigunguti  kwa  Tambi  amesema ubovu wa barabara umepelekea  maji kujaa barabarani hivyo wananchi kuwa hatarini dhidi ya magonjwa  ya mlipuko kama Kipindu Pindu.

Kwa upande wake mmoja wa Dereva wa Daladala  anayetumia barabara hiyo amesema vyombo vyao usafiri kama magari na daladala yamekua yakiharibika mara kwa mara kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuiomba Serikali kushughulikia kadri iwezekanvyo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni