Maisha

Tamasha la Wanawake Wajasiriamali kufanyika Dar

Tarehe September 27, 2017

Mwenyekiti na mjumne wa kamati ya maandalizi ya tamasha la 11 la Wanawake Wajasiriamali(MOWE) Bi.Anna Matinde akieleza jambo kwa waandishi wa habari Jijini dar es salaam katika ukumbi wa idara ya habari maelezo juu ya tamasha hilo.

Umoja wa wanawake wajasiriamali (MOWE) wameandaa tamasha  la 11 kwa wajasiriamali litakalofanyika kuanzia tarehe 24-30 oktoba , 2017 katika viwanja wa mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam lengo ikiwa ni kupanua wigo wa masoko pamoja na kuonyesha bidhaa na fursa mbalimbali za kijasiriamali zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa kamati ya tamasha hilo, Bi. Zubeda Kiluwa amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa na kauli mbiu isemayo‘Mwanamke mjasiriamali funguka shiriki kujenga Tanzania ya viwanda’

“Tunawaalika wanawake wote popote walipo kushiriki maadhimisho na maonyesho haya kwani yatawahusiha wadau mbalimbali wa maendeleo ya wanawake, Wizara pamoja na taasisi za serikali na mashirika binafsi,”alisema Kiluwa.

Tamasha hilo litafunguliwa  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage ambapo wadau watakaoshiriki  kutoa elimu za kijasiriamali katika tamasha hilo ni pamoja na Wakala wa Usajili Biashara na utoaji  leseni (BRELA), TRA, GSM, SIDO, TBS, TFDA pamoja na wawakilishi kutoka  katika benki mbalimbali   ambao kupitia semina hiyo watatoa elimu juu ya ujasiriamali.

Aidha Bi.kiluwa ameleza kuwa gharama zitakazotozwa kwa wajasiriamali watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni shillingi 50,000 kila mmoja, na kwa yeyote atakayeshiriki kwaajili ya uzinduzi, ununuzi na kujionea bidhaa mbalimbali hawatatozwa gharama yoyote.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya tamasha hilo Bi.Anna Matinde amaesema kuwa tamasha hilo halitawahusisha wajasiriamali peke yake bali litawahusisha watu wote lengo likiwa ni kubadilishana mawazo ya kimaendeleo katika kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda.

 

[nafasi_ya_tangazo_la

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni