Maisha

Serikari yaja na maamuzi mapya kuhusu miradi ya Wananchi Vijijini

Tarehe July 29, 2017

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene.

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene.

Serikali imekusudia kurejesha mfuko wa Maendeleo ya Serikali za mitaa, lengo likiwa ni kuinua miradi mbalimbali inayoanzishwa na wananchi vijijini mwao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa mfuko wa maendeleo ya serikali za mitaa katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe.George amesema kuwa miradi hiyo ina umuhimu mkubwa sana katika kuinua uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa, wananchi wamekua wakiibua miradi kama vile kujenga barabara, zahanati,nyumba za walimu na madarasa ambayo imekuwa ikianzishwa  na wananchi baadae kuendelezwana Serikali.

Aidha Mhe. George alisema kuwa miradi imekuwa ikichangiwa na serikali ambapo katika bajeti iliyopita ilitenga kiasi cha fedha takribani billion 156 kwaajili ya miradi, lakini kwa mwaka huu wa fedha serikali imetenga kiasi cha fedhaTsh billion 249, hivyo imeamua kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili kuchangia mfuko wa miradi hiyo na kuhuisha miradi iliyokuwa imeachwa bila kumalizika.

Kwa upande wake naibu waziri wa fedha na mipango Dkt.Ashatu Kijaji amesema kuwa wamebadilisha mfumo uliokuwa mwanzo ili kuuboresha Zaidi katika kuweka na kupima mfumo mzima lengo ni kuzifanya Halmashauri zifanye kazi zenyewe na waweze kukusanya kodi ya kutosha kwani Hakuna maendeleo yoyote yale yanayoweza kufanyika bila kuwepo kwa bajeti ya fedha.

Dkt.Kijaji aliongeza kwa kusema kuwa watanzania wanapaswa kufuata kauli ya Mhe. Rais ya kujitegemea wenyewe hivyo halmashauri zinapaswa kufanya kazi kwa bidi ili ziweze kujitegemea zenyewe pasipo kuwategemea zaidi wadau wa maendeleo.

Naye Bw. Lin Zhiyong ambae ni mwakilishi wa ubalozi wa china amesema kuwa miradi hiyo ina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha  maendeleo ya mikoa na Serikali kwa ujumla, kwakuwa kila mkoa umeonekana kuwa na vipaumbele katika sekta tofauti tofauti kama kilimo, utalii na miundombinu, hivyo Serikali kuu inapaswa kusaidia Serikali za mitaa ili kuvutia uwekezaji wa nje.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni