Biashara

Nguo za watoto zapanda bei kuelekea Sikukuu ya Iddi

Tarehe June 13, 2017

77

nafasi_ya_tangazo_la1]

Bei ya nguo za watoto imetajwa kupanda kuelekea Sikukuu ya Idd suala ambalo huenda likawakwamisha watu wa hali ya chini kununua bidhaa hiyo.

Wakiongea na mtandao huu, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam , Wamesema kumekuwa tabia kwa  sasa kwa Wafanya Biashara kUpandishia bei kiholela kitu ambacho kinawaumiza Wananchi wa kawaida.

“Kumekuwa na tabia  ya upandishwaji wa nguo za watoto kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Iddi mara kwa mara na kuwakosesha baadhi ya watu kupata mahitaji ya nguo kwa manufaa ya watu wachache.”amesema Mary mkazi wa Kinondoni.

Nao baadhi ya wafanya biashara wa kutoka katika soko la Kariakoo,Karume,Temeke na manzese Wamesema inawalazimu kupandisha bei kutokana na uhitaji mkubwa wa bidhaa hizo za nguo msimu wa Sikukuu.

Naye Juma Mrisho mkazi wa Temeke ameiomba Serikali kukabiliana na wafanyabiashara wanaopandisha bei ili kupata faida kitu ambacho kinawaumiza wananchi wa kawaida.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni