Maisha

Mgombea Ubunge awataka wanawake kususia ‘ngono’ akiomba kura

Tarehe August 1, 2017

Moja ya Kituo cha kupigia kura nchini Kenya.

Moja ya Kituo cha kupigia kura nchini Kenya.

Wakati  siku za kufanyika kwa  uchaguzi mkuu nchini Kenya zikihesabika,Mgombea Ubunge ambaye ni Mwakilishi wa Wanawake wa jimbo la Mombasa na anayewania ubunge wa eneo la Likoni Mishi Mboko amewataka wanawake kuwanyima ‘unyumba’ wanaume wasio jiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Mgombea huyo alitoa wito huo kwa wanawake waliopo katika maeneo yenye wafuasi wengi wa upinzani nchini Kenya katika moja ya kampeni zake.

Tendo la ngono limekuwa likiibuliwa katika siasa nchini Kenya, wengi wakilitazama kama njia inayoweza kuwaongezea nafasi ya kushinda.

Wanasiasa  mbalimbali   wamekua  wakijaribu kuhamasisha watu kujiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni