Maisha

Mbunge adai kumnyima mwanaume tendo la ndoa ni dhuluma kubwa

Tarehe July 27, 2017

o-COUPLE-APART-BED-facebook

Mbunge mmoja nchini Malaysia amekosolewa vikali baada ya kusema kuwa wanawake wanaowanyima waume/mabwana zao tendo la ndoa huwasababishia dhuluma za kisaikolojia.

Mbunge huyo, Che Mohamad Zulkifly Jusoh, kutoka chama tawala cha Barisan Nasional, alikuwa akizungumza wakati wa mjadala wa bunge kuhusu dhuluma za nyumbani.

Malaysia iko katika mikakati ya kufanyia sheria marekebisho kutatua dhuluma za nyumbani.

Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 58 kutoka Jimbo la Terengganu, amesema kuwa wanaume wanapitia kwa asilimia kubwa dhuluma za kisaikolojia kuliko zile za kimwili.

“Licha ya wanaume kuwa wenye nguvu kuliko wanawake, wanawake huwadhulumu katika masuala kama haya kwa njia iliyo ya kuumiza zaidi,” amesema Jusoh.

Wanasiasa na makundi ya wanaharakati wana matumaini kuwa mswada mpya utawakinga zaidi waathiriwa wa dhuluma za nyumbani.

Aidha, Bwana Che aliliambia bunge kuwa kumnyima mwanaume muislamu haki ya kuoa mke wa pili ni sawa na kumdhulumu.

Nchini Malaysia, nchi yenye wasilamu wengi ni halali kwa wanaume kuoa hadi wake wanne ikiwa tu watapata idhini kutoka mahakama za sharia.

.

Continue with more paragraphs …

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni