Maisha

Kivutio kingine cha Watalii chagunduliwa kilimanjaro

Tarehe June 5, 2017

mti

Pamoja na kuwepo kwa vivutio vingi vya utalii hapa nchini, Serikali imetangaza kuwepo kwa mti mrefu  zaidi barani Afrika.

Mti huo aina ya Mkukusi  una urefu wa mita 81.5 unapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) ambapo una umri wa zaidi ya miaka 600 hadi hivi sasa.

Charles Ngendo ambaye ni Mhifadhi wa  utalii katika Hifadhi hiyo amesema hifadhi inatarajia Mti huo  kuwa kivutio cha utalii mbacho kitaiingizia Serikali  fedha za kigeni.

Aidha pamoja na changamoto za kuchelewa kufika Mrusungu ambapo mti huo upo KINAPA inatarajia kuboresha miundombinu  ili kuwawezesha watalii kufika.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni