Habari/News

Zuma akaliwa kooni,apewa saa 48 kujiuzulu

Tarehe February 13, 2018

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo.

Kwa mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC.

Duru zinasema ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madaraka.

Rais Jacob Zuma  anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa pia  alishindwa uongozi wa chama tawala Desemba mwaka jana.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni