Habari/News

Zitto kabwe atema Cheche akifichua siri ya ujio Muswada tata

Tarehe October 13, 2017

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli imetajwa kudhamiria kuuwa vyama vya upinzani nchini kufuatia muswada wa sheria ambao umesambazwa kwenye vyama vya siasa.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe na kubainisha kuwa muswada huo ambao umesambazwa tayari kwa vyama vya siasa ni kama hukumu ya kuviuwa vyama vya upinzania nchini kwani kuna vifungu ambavyo vinakataza vyama vya siasa kisheria kufanya mikutano ya hadhara isipokuwa mwaka wa uchaguzi tu, lakini pia watu wanaoruhusiwa kufanya mikutano hiyo ni wabunge na madiwani tu kwenye majimbo yao husika.

Amesema kuwa hawatakubali jambo hilo na watapinga sheria hiyo ndani ya Bunge pamoja na nje ya bunge na kusema wao watalinda mfumo wa vyama vingi nchini kwa gharama yoyote kwani uwepo wa vyama ni haki Kikatiba.

Kwa habari zaidi soma maoni ya Zitto Kabwe hapa…………

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni