Habari/News

Zitto Kabwe afichua mateso ya raia kwenye vituo vya Polisi

Tarehe February 25, 2018

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini , Mhe. Zitto Kabwe.

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini , Mhe. Zitto Kabwe amefichua mateso wanayopata raia wakiwa wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini.

Akizungumza na Wandishi wa habari Zitto amesema akiwa rumande amemshuhudia kijana ambaye amevunjwa mbavu kituoni na hajapelekwa kutibiwa suala linalohatarisha usalama wake.

Amesema  kitendo cha yeye kukamatwa na kulazwa ndani kwa siku moja kumemfanya agundue kuwa kuna Watanzania wengi wanateseka na kupata shida kwenye vituo vya polisi nchini.

“Watanzania wanateseka sana chini ya mikono ya polisi, sheria inataka ndani ya masaa 48 polisi wame wamewafikisha mahakamani watuhumiwa lakini tumekutana na watu wamekaa ndani siku 3 hata maelezo tu hawajaandika, wengine wana siku 20 wapo ndani hawajafikishwa mahakamani” alisema Zitto Kabwe

Kiongozi huyo amesema polisi wamekuwa wakiwatesa wananchi ndani ya vituo hivyo vya polisi na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watuhumiwa bila kuwapeleka hospitali kwa matibabu.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni