Habari/News

Zitto aifungukia DARUSO hosteli za UDSM kupatwa na ufa

Tarehe December 4, 2017

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe, amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutoa tamko kufuatia kusambaa kwa picha zinazodaiwa kuwa ni za Hostel Mpya za wanafunzi hao zikiwa zimetengeneza nyufa ikiwa ni miezi kadhaa tu imepita tangu kuzinduliwa rasmi na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto amefunguka yafuatayo;

“DARUSO mpo wapi? Mnasubiri kucheleweshewa mikopo ndio mseme? Au mnasubiri majengo yaanguke na madhara yatokee? Wajibu wa Serikali ya Wanafunzi ni pamoja na kusemea mambo ya hovyo yanayofanyika. DARUSO mnapaswa kutoa statement kuhusu ukweli wa Habari hizi za mabweni ya wanachama wenu, Wanafunzi. Mabweni haya yamegharimu shilingi 59 bilioni ( achaneni na porojo za 10bn ) hivyo ni lazima msimame kuhoji. Pia uchunguzi huru ufanyike kwa hostels zote zilizojengwa na TBA ili kulinda uhai wa Wanafunzi wetu.

Nitashangaa sana kuona Vijana wa Vyama vya siasa wanakaa kimya kwenye jambo kama hili.”

Hatahivyo, Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo, Mhandisi Elius Mwakalinga amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za kweli na kwamba kupasuka huko ni kawaida kwa majengo makubwa hivyo watu wasiwe na hofu.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni