Habari/News

Zitto adai agizo la Tume ya Uchaguzi halitekelezeki

Tarehe November 14, 2017

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.

Ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwataka wanasiasa kujikita katika kuwanadi wagombea wa chaguzi ndogo za madiwani na sio vinginevyo, chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Kiongozi wake, Mhe. Zitto Kabwe kimesema kuwa hilo haliwezekani.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameandika yafuatayo;

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC ) inasema tusiongee tofauti na kunadi wagombea kwenye kampeni. Hili haliwezekani.

Sisi ACTWazalendo kwa mfano kama Chama tuliamua kuwa na ujumbe wa jumla kwenye chaguzi hizi, HAKI na UCHUMI. Tunakwenda kwenye kata kuwaeleza wananchi namna kura yao ina thamani na watume ujumbe kwa Serikali kuwa hawapendi kuona haki za msingi za wananchi zinaminywa na hali zao za maisha kuwa mbaya siku hadi siku kutokana na Uendeshaji mbovu wa Uchumi.

Tunaeleza haya kwa mifano halisi ya eneo tunalogombea. Tumetuma watafiti kila eneo na tunahusisha masuala ya kitaifa na kwenye husika. Hivyo haiwezekani sisi kufuata maelekezo ya Tume. Kutuelekeza hivyo ni sawa na kututaka tusifanye kampeni.”

Mapema jana, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistolces Kaijage alivitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya Uchaguzi  kuelekea Uchaguzi mdogo wa madiwanina kutaka kampeni hizo kujikita katika kumnadi mgombea husika tu.
Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017 ambapo wapiga kura 333,309 wanategemewa kupiga kura siku ya uchaguzi huo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni