Habari/News

Zitto acharuka wabunge 9 UKAWA kutajwa kuhamia CCM

Tarehe December 6, 2017

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe (kushoto), pembeni ni Tundu Lissu.

Baada ya taarifa yenye kichwa cha habari ‘Wabunge Tisa UKAWA Watajwa Kuhamia CCM’, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo ameibuka na kuwataka wenzake wasirukwe na akili na kutumia hali hiyo kwa maslahi ya kisiasa ndani ya vyama vyao.

Zitto ameandia yafuatayo asubuhi ya leo;

“Nimesoma kuhusu inayoitwa wabunge 9 wa CHADEMA na CUF kwenda CCM. Kwa uzoefu wangu wa siasa za Tanzania (yalinikuta) ninanusa harufu ya propaganda. ‘ mpe mbwa jina baya umuue ‘ ndio kinachoendelea. Ni siasa za kipuuzi sana zinazoendelea. Ninawaombea sana wenzangu wasirukwe akili na kutumia sintofahamu ya hali ya siasa kwa maslahi ya kisiasa ndani ya vyama vyao. Nchi hii inahitaji kulinda mfumo wa Vyama vingi. Hebu kueni na mtazame maslahi mapana ya Demokrasia.

Acheni utoto.”

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni