Habari/News

Zitto aandika mazito kwa JPM Rugemarila na Harbinder Seth wakiburuzwa mahakamani

Tarehe June 19, 2017

Magufuli-na-Zitto

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Mhe Zitto Kabwe kupitia kurasa zake za Facebook na Twitter leo ameandika machache kumuhusu Rais Magufuli muda mfupi baada ya wanaofahamika kama vigogo wa sakata la ESCROW, Mfanyabiashara, James Rugemarila na Mmiliki wa PAP, Harbinder Seth kufikishwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Zitto ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipiga kelele kuhusiana na ufisadi wa IPTL/PAP na sakata la Escrow ameandika yafuatayo;

“Rais Magufuli nimekuwa nakupinga kwenye mambo mengi, na nitaendelea kukupinga, lakini kwenye hili la IPTL umetendea nchi haki. Hongera sana.” Ameandika.

“Leo ninaona vita dhidi ya ufisadi ina maan kubwa. Kumkamata Harbinder Singh Seth na kumfikisha mahakamani ni hatua kubwa ya kupongezwa,” ameandika tena Zitto.

19225668_1450057345073521_2361555767960450934_n

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni