Habari/News

Whamiaji haramu wengine 83 wakamatwa Iringa

Tarehe February 25, 2018

Wahamiaji haramu  83 wamekamtwa  mkoani Iringa huku dereva aliyekuwa akiwasafirisha akifanikiwa kutoroka.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Hope Kawawa alisema Whamiaji hao  walikamatwa juzi saa kumi na moja jioni karibu na bomba la mafuta la Tazama.

Amesema Wahamiaji hao walikamatwa wilayani Kilolo mkoani hapa wakiwa safarini kupelekwa Malawi kisha Afrika Kusini.

“Hata hivyo katika harakati za kukamatwa kwao, dereva wa lori mali ya mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya alitoroka.”Amesema Hope Kawawa

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni