Habari/News

Waziri wa Magufuli apiga Marufuku kodi ya Mwaka

Tarehe December 6, 2017

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.

Serikali ya awamu ya tano kupitia  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  amesema wamiliki wa nyumba kuanzia sasa wanatakiwa kulipwa kodi ya mwezi mmoja mmoja.

Lukuvi amesema hayo wakati akifungua jengo la ofisi ya makao makuu ya shirika la nyumba nchini (NHC) na kubainisha  kuwa kila mmiliki wa nyumba anapaswa kumpa fulsa mpangaji kulipa kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya miezi sita au mwaka.

“Mpangaji anatakiwa kulipa kodi kila mwezi labda awe ametaka mwenyewe kulipa miezi sita au mwaka kama uwezo wake unaruhusu kufanya hivyo”, amesema Lukuvi.

Lukuvi amesisitiza kuwa wamiliki wa nyumba kuanzia sasa wanatakiwa kulipwa kila mwezi, ili iwape fursa wapangaji kuwa na maisha yanayowezekana kuishi maeneo ya mjini.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni