Habari/News

Waziri Mkuu awapa majukumu mazito Ernest Mangu,Mumwi

Tarehe April 9, 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchini Urusi na Rwanda  kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuwavutia wawekezaji.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na Balozi Ernest Mangu anayewakilisha Tanzania nchini Rwanda na Balozi Simon Mumwi anayewakilisha Tazania nchini Urusi, katika ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.

Majaliwa  amesema  Mabalozi hao wanatakiwa  kila mwisho wa mwaka wajifanyie  tathmini ya mafanikio waliyoyapata kutokana na uwakilishi wao katika Mataifa ambayo  ni kwa kiasi gani wamechangia kwenye uboreshaji wa maendeleo ya Taifa.

Mbali na kutangaza sekta ya utalii,Waziri Mkuu pia  amewataka watafute wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta nyingine kama vile madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni