Afya

Waziri azungumzia nchi kukumbwa na uhaba wa dawa

Tarehe November 8, 2017

Dawa ztajwa kuadimika.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Afya, Jinsia, watoto na wanawake Mheshimiwa Ummy Mwalimu, imesema kwa sasa nchi haina tatizo la upungufu wa madawa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Mwalimu alisema hayo wakati  akijibu swali la Waziri Kivuli wa Afya, Mhe Dr Godwin Mollel Bungeni mjini Dodoma, na kusema kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. John Pombe Magufui, imehakikisha imeongeza bajeti ya dawa ili kuinua sekta ya afya nchini.

Kwanza nataka kumsahihisha waziri kivuli jambo moja, hakuna upungufu mkubwa wa dawa Tanzania, na kati ya jambo kubwa ambalo Rais amelifanya ni kuongeza bajeti ya dawa, tusikariri taarifa zilizopitwa na wakati, kama mnataka kumtendea haki Rais Magufuli, mtendeeni kwa kumpima ni kiasi gani amewekeza katika upatikanaji wa dawa”, amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema kwa sasa serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha inakabiliana na kutoingiza dawa ambazo zinakaribia kuharibika, na kuingia hasara kuziteteketeza huku ikisema changamoto kubwa huwa inajitokeza kwa dawa za misaada, kitu ambacho wameshaacha kufanya hivyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni