Habari/News

Waziri avunja ukimya,ni kuhusu maandamano ya Mange Kimambi

Tarehe April 11, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama ametoa ushauri kuhusu maandamano na kudai kuwa mtu yoyote ambaye ana ratibu maandamano lazima afuate sheria.

Jenista Mhagama amesema hayo bungeni ambapo amebainisha kuwa  kama kila mtu ataamua kuandamana kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu hilo litakuwa jambo ambalo si sawa hivyo amevitaka vyama vya siasa kufuata sheria za nchi na si kuvunja sheria za nchi.

“Katiba yetu imeruhusu maandamano lakini maandamano yameratibiwa kisheria na kama yameratibiwa kisheria lazima tuhakikishe kwamba tunazingatia sheria katika kuratibu maandamano nchini kwetu Tanzania”Amesema Mhagama.

Mwanaharakati Mange Kimambi amekua akihamasisha maandamano akidai kuwa serikali imeshindwa kukabiliana na mambo kadhaa ikiwemo Polisi kuua raia,utekaji  na kuwepo ukosefu wa ajira.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni