Habari/News

Waziri atoa siku 14 kiwanda cha Dangote kitoe Mikataba

Tarehe January 22, 2018

Kiwanda cha Dongete Mtwara.

Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko imetoa siku 14 kwa uongozi wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa gypsum.

Kauli  ya Biteko inafuatia kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na uongozi ambapo amesema mikataba hiyo inapaswa kuwa na kipengele cha kuwalipa ndani ya siku 30 baada ya kiwanda kukusanya gypsum kutoka kwa wachimbaji hao, lengo likiwa ni kuleta ufanisi na tija katika biashara zao.

Uamuzi wa Biteko unafuatia wachimbaji hao  kulalamikia kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka kiwandani bidhaa zao hivyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni