Habari/News

Waziri ‘amtumbua’ Kigogo aliyemdanganya Rais Magufuli

Tarehe February 26, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Msimamizi wa mradi mkubwa wa maji katika kata ya Nguruka wilayani Kigoma Erick Suma amesimamishwa kazi kudanganya kuhusu kuhusu mradi wa Maji wilayani humo.

Uamuzi huo umechukuliwa na Waziri wa maji Mhandisi Isaac Kamwele na kubainisha kuwa amechukua uamuzi huo kufuatia kutokamilika kwa mradi wa maji ambao uliokuwa ukamilike mwezi Disemba mwaka jana lakini  haujakamilika hadi sasa

Waziri Kamwele ambaye ametembelea mradi huo amesema msimamizi huyo wa mradi alimdanganya rais alipotembelea mradi huo mwezi wa saba mwaka jana kwa kutoa ahadi ya kukamilika kwa wakati mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni tatu .

Kamwele  ameongeza kwamba licha ya msimamizi huyo kulipwa fedha zote anazodai kwa mujibu wa mkataba lakini kazi inakwenda taratibu na kuathiri maisha ya wananchi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni