Habari/News

Watumiaji wa Airtel Kuneemeka Msimu wa Sikukuu

Tarehe November 21, 2017

 Mkurugenzi mawasiliano Airtel Beatrice Singano (kulia) akiwa na Isack Nchunda Mkurugenzi Masoko

Wakati msimu wa sikukuu ya krismasi umewadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeupokea msimu huo kwa kuendelea kuwanufaisha  wateja pamoja na mawakala wa huduma ya Airtel Money nchi nzima kwa  kuwagawia  gawio la shilingi bilioni 2  kutokana na  utumiaji wao wa huduma ya Airtel Money.

Taarifa kutoka kampuni hiyo leo ikiwa na kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso imethibitisha kuwa gawio la faida kutokana na huduma ya Airtel Money hutolewa katika kila robo ya mwaka ambapo gawio la awali lilianza kutolewa Mwaka 2015 na hadi kufikia leo jumla ya shilingi bilioni 11.8 zimeshagawiwa kwa wateja wa Airtel Money.

“Tunapoingia katika shamrashamra za msimu wa sikukuu, Airtel tunatambua  umuhimu wa kuwazawadia wateja wetu, tunafurahia kuona tuko katika wakati sahihi kwa kutoa gawio hili ili kutoa fursa kwa wateja wetu kuweza kutumia wakiwa na familia au wawapendao kwa kujipatia mahitaji yao muhimu ndani ya msimu wa sikukuu”.

Gawio hili la Airtel Money linaloaanza kutolewa leo linalotokana na faida iliyopatiikana kuanzia ya robo mwaka kuanzia mwezi Juni hadi Septemba 2017, ambapo watakaofaidika ni wateja wote wanaotumia huduma ya Airtel Money pamoja na mawakala wake nchini nzima. 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni