Habari/News

Watu zaidi ya 30 wajeruhiwa wakipinga msimamo wa Marekani

Tarehe December 8, 2017

Wakati Tanzania ikisisitiza kuwa itaendelea kuutambua Mji wa Tel Avivi kama Mji Mkuu wa Israel kuwa na makao ya ubalozi wake tofauti na Marekani ambayo imeutangaza Mji wa Yerusalemu kama Mji Mkuu wa Israel na kuagiza kuhamishwa kwa ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Yerusalemu, watu, Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza na ukingo wa magharibi ambapo zaidi ya wapalestina thelathini wamejeruhiwa katika makabiliano na polisi wa Israel.

Waandamanaji wameripotiwa kuchoma matairi na kurusha mawe huku maafisa usalama wa Israel wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira. huku Wapalestina wakiamua kuzima taa za Krismasi kwenye Mji Mtakatifu wa Bethlehem alikozaliwa Bwana Yesu, kupinga hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutambua Mji wa Yerusalemu kama Mji Mkuu wa Israel.

Afisa Habari wa Manispaa ya Bethelehem, Fady Ghattas amesema Mti wa Krismasi ulioko kwenye kanisa la Bethlehem ambako wakristo huamini Bwana Yesu alizaliwa, ulizimwa taa zake kwa amri ya Meya wa Manispaa hiyo.

Miji mingine iliyozimwa taa ni Ramallah ulio karibu na mahali alipozikwa kiongozi wa zamani wa Palestina Yasser Arafat.

Waarabu na waislamu katika nchi za Mashariki ya Kati ikiwemo Saudi Arabia, wamepinga hatua ya Trump ya kutangaza kutambua Yerusalemu kuwa Mji Mkuu wa Israel.

Hii ni kufuatia Rais Donald Trump kutangaza kuutambua Mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni