Habari/News

Wananchi wavamia tena mgodi wa Acacia North Mara

Tarehe June 19, 2017

mgodini-1

Kundi kubwa la wananchi kutoka vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa Acacia North Mara wamevamia mgodi huo tena leo.

Wananchi hao wanadaiwa kuendelea kukusanyika kwa wingi katika lango la mgodi huo maarufu ‘Boom Gate’ huku Jeshi la Polisi likijaribu kuwatawanya.

Tukio hilo linajiri kwa mara ya pili baada ya hapo jana kundi la wananchi zaidi ya 400 kuvamia mgodi wa dhahabu wa North Mara, Wilayani Tarime wakidai malipo ya fidia.

Wakazi hao ni kutoka katika baadhi ya kata zinazopakana na mgodi huo ambao maeneo yao yalifanyiwa tathmini tangu mwaka 2014 bila kulipwa hadi sasa na kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha hiyo hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Adrew Sata alithibitisha kutokea kwa jaribio hilo la kuvamia mgodi huo uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Katika tukio hilo, hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala kushikiliwa na polisi.

Ndugu msomaji endelea kutembelea mtandao wako wa hivisasa.co.tz kwa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni