Habari/News

Wananchi wavamia mgodi wa North Mara

Tarehe June 19, 2017

Mgodi

Kundi la wananchi zaidi ya 400 jana walivamia mgodi wa dhahabu wa North Mara, Wilayani Tarime wakidai malipo ya fidia.

Wakazi hao ni kutoka katika baadhi ya kata zinazopakana na mgodi huo ambao maeneo yao yalifanyiwa tathmini tangu mwaka 2014 bila kulipwa hadi sasa na kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Adrew Sata amethibitisha kutokea kwa jaribio hilo la kuvamia mgodi huo uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Katika tukio hilo, hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala kushikiliwa na polisi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni