Habari/News

Wananchi Burundi wapiga kura kuongeza muda wa Urais

Tarehe May 17, 2018

Burundi inapiga kura ya maamuzi  yenye lengo la kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba.

Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka wa 2034.

Kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi huo na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani.

Rais Pierre Nkurunziza amekuwa akipiga kampeni nchini humo, akisema kwa  kuwa katiba hiyo itakua na manufaa kwao.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni