Habari/News

Waliojiuzulu Chadema,wateuliwa kugombea Ubunge CCM

Tarehe January 6, 2018

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole.

Wabunge wawili waliojiuzulu nafasi zao za ubunge na kutimkia chama cha Mapinduzi(CCM) ambao ni Dk Godwin Mollel na Maulid Mtulia wameteuliwa kugombea ubunge kwa mara nyingine katika majimbo ya Siha na Kinondoni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole imesema kuwa baada ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dk Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro na Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Taarifa  hiyo imeongeza kuwa wagombea wa ubunge wanaelekezwa kufika katika ofisi za CCM katika mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM wa mikoa hiyo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni