Afya

Wagonjwa wabeba neti,Mashuka kutibiwa Hospitali ya Mkoa

Tarehe October 17, 2017

Wagonjwa watakiwa kubeba mashuka hospitalini.

Uhaba wa mashuka,neti na mablanketi umepelekea  wagonjwa mkoani Hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kulazimika kwenda na vifaa hivyo kutoka majumbani kwao ili kujinusuru na mbu pamoja na baridi nyakati za usiku.

Akizungumzia suala hilo Kaimu Mkurugenzi wa Kahama mji Bi. Flora Sangiwa amesema uchakavu wa miundombinu ya matibabu katika hospitali ya Kahama, unachangiwa na ufinyu wa bajeti inayotengwa lakini pia hospitali inahudumia wagonjwa wengi kutoka nje na ndani ya wilaya hiyo.

Kwa upande wake  Mganga mfawidhi wa hospitali ya Kahama Dr. Fredrick Malunde amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na nyinginezo zinazoikabili hospitali hiyo, ambapo pia amesema hospitali imeelemewa na wagonjwa wanaolazwa kwa idadi ya 30,000 kwa mwezi, huku kukiwa na wastani wa wagonjwa 200 wanaolazwa kwa siku.

Wadau mbalimbali wametakiwa  kujitokeza kusaidia vifaa hivyo ambapo kwa sasa Benki ya Posta Tanzania tawi la Kahama wametoa mashuka 100 na vyandarua 50.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni