Habari/News

Wadaiwa sugu Bodi ya Mikopo wapewa kibano zaidi

Tarehe October 13, 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo.

Halmashauri 12 ambazo ni wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa zimetakiwa kuwa zimerejesha deni la Shilingi bilioni 2 kabla ya Desemba 30, mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa agizo hilo na kutaja Halmashauri hizo kuwa ni Mwanza, Mbeya, Moshi, Singida, Kigoma, Karatu, Mbinga, Pangani, Mbinga, Morogoro, Igunga na Kongwa.

Amesema hadi Septemba 30 bodi imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.7 kwa halmashauri 54 nchini lakini fedha zilizorejeshwa ni Shilingi bilioni 6.6.

“Halmashauri nyingi zimejitahidi kurejesha mikopo kwa wakati lakini kuna zilizoonyesha usugu katika kurejesha mikopo,” amesema.

Amesema kutorejeshwa kwa mikopo kunasababisha halmashauri nyingine kukosa fursa ya kukopa.

Jafo ameiagiza bodi kuangalia utaratibu wa kupitisha mikopo inayolenga ujenzi wa viwanda na uwekezaji katika halmashauri ili kukuza ajira na uchumi wa viwanda.

“Bodi iache kubweteka, ijipange kimkakati  kujenga uwezo mkubwa wa kutoa mikopo kwa halmashauri zilizo makini katika mapinduzi ya viwanda,” amesema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni