Habari/News

Vifaru vyaonekana vikikatiza Jijini Harare

Tarehe November 14, 2017

Vifaru vinne vimeripotiwa kuonekana vikikatza mitaa na kuelekea katika Mji Mkuu wa Harare, ikiwa ni siku moja tu kupita baada ya Mkuu wa Majeshi nchini humo, Constatino Chiwenga kutangaza kuwa atalazimika kuingilia kati kijeshi na kumaliza mzozo ndani ya chama cha ZANU-PF.

Mgogoro huo unatokana na Rais Robert Mugabe kumfukuza aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa pamoja na wanachama wanaomuunga mkono ambao kwa mujibu wa Chiwenga ni watu muhimu waliopigania uhuru kutoka kwa walowezi wa kizungu huku Jeshi likidaiwa kuwa limekuwa likimuunga mkono Mnangagwa kumrithi Rais Mugabe mwenye miaka 93 sasa.

Hatahivyo, mke wa Rais Mugabe, Grace ameibuka na kuwa mshindani mkubwa wa Mnangagwa ambaye baada ya kufutwa kazi Mnangagwa alilazimika kukimbilia uhamishoni huku wadadisi wa mambo wakidai kuwa kuna shinikizo kutoka kwa Bi. Grace Mugabe juu ya hatua hizo.

Wakati huohuo, vijana wa chama tawala cha ZANU-PF wamemkosoa Jenerali huyo wa Jeshi mwenye cheo cha juu zaidi nchini humo kufuatia kauli yake na kudai kuwa mkuu huyo wa jeshi haungwi mkono na jeshi lote.

Tayari chama cha Upinzani nchini Zimbabwe, MDC kimepuuzilia mbali kauli hiyo pia kikidai kuwa Jenerali huyo ni mtu asiye na nguvu zozote.

Matamshi hayo yanajiri kufuatia hatua ya Chimwenga kutishia kufanya mapinduzi iwapo chama cha Zanu-PF hakitasita kuwafukuza wapiganaji wa uhuru katika chama hicho ambao wametofautiana na Rais, Robert Mugabe na Mkewe Grace Mugabe.

“Hana nguvu zozote kumzuia Grace kuwatukana wapiganaji wa uhuru wa zamani,” Msemaji wa MDC Kuraoune Chihwaye alinukuliwa akisema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni