Habari/News

Video za ‘utupu’ zamchefua rais Magufuli

Tarehe December 12, 2017

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Video za utupu za wasanii nchini zimemchefua rais Dkt John Pombe Magufuli na kuzitaka mamlaka zinazohusika na maadili kuchukua hatua dhidi ya wasanii hao.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akufungua mkutano mkuu wa tisa wa jumuiya ya wazazi CCM utakaofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

Katika hotuba yake Rais Magufuli amehoji vyombo vya habari, wasimamizi wa maadili, wizara na taasisi zinazodhibiti kama zimeshindwa kushughulikia maadili ya vijana.

“Hii ni jumuiya ya wazazi lakini maadili yameanza kupotea na jumuiya ipo kwa ajili ya kukemea, mimi nimekuwa shabiki mzuri wa muziki, wanaovaa utupu ni wanawake, wanaume wanacheza wakiwa wamevaa, sana sana wataachia kifua wazi tu ili waonekane ‘six pack’, lakini wanawake, walio wengi wanaachia viungo vyao,”Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema wakati umefika bila kujali itikadi za vyama kuungana katika ujenzi na ulinzi wa maadiili ya Watanzania.

Mtindo wa kucheza muziki kwa utupu ulianza kuota mizizi Tanzania tangu wanamuziki walipoa anza kuiga aina hiyo ya uchezaji kutoka nchi ulaya ambako baadhi ya wasanii wake wa kike hucheza muziki kwa kuonesha baadhi ya maungo ya ndani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni