Habari/News

Video: Maandamano ya wananchi kupinga kichapo cha FFU

Tarehe October 25, 2017

Baadhi ya wananchi katika maandamano Ukonga Dar.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewapiga marufuku askari wa kikosi cha FFU na kusema hataki kuwaona wakisumbua wananchi katika eneo la Ukonga Dar es Salaam na kutaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa kitendo walichofanya kuwapiga wananchi.

Sophia Mjema amesema hayo alipowatembelea wananchi hao ambao wamelalamika kufanyiwa fujo na kupigwa na askari hao kwa siku mbili kutokana na askari mmoja kuuawa na watu wasiojulikana.

Ameongeza kuwa   askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni watu gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya fujo na kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni