Habari/News

Uzalendo wamshinda Rugemarila amuomba DPP amtaje Mwizi wa Escrow

Tarehe December 22, 2017

Mshtakiwa wa kesi ya utakatishaji fedha James Rugemarila,(kulia).

Uzalendo umetajwa kumshinda Mshtakiwa wa kesi ya utakatishaji fedha James Rugemarila ambapo ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili kutoa ushahidi wake ni nani haswa anayetakiwa kukamatwa katika kesi hiyo.

Rugemalira amesema hayo Baada ya kesi hiyo kusikilizwa tena leo, mshtakiwa James Rugemarila akiwa sambamba na mshtakiwa mwenzake kwenye kesi hiyo amesema anaushukuru upande wa mashtaka kwa kumpeleka kufanya mahojiano na kumrudisha salama gerezani, na kuongeza kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo

Kufuatia ombi hilo Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi alimtaka kuwasiliana na mwanasheria wake ili kuandika barua ya kwenda kwa DPP, na kuahirisha kesi hiyo mpaka January 5, 2018, ambapo itasikilizwa tena kutoka na upelelezi kutokamilika.

Vigogo hao akiwemo Rugemarila na mwenzake Harbinder Singh Sethi  wanashtakiwa kwa kuhujumu uchumi na utakatishaji fedha na kuiingizia serikali hasara ya milioni 309.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni