Habari/News

Ukatili watoto wa Kike bado changamoto Singida na Dodoma

Tarehe November 13, 2017

Koshuma Mtengeti Mkurugenzi CDF 

Tatizo la Ndoa za Utotoni katika Mkoa wa Tabora limezidi kuwa changamoto huku Mkoa wa Manyara ukiwa unakabiliwa na changamoto ya masuala ya Ukeketaji kwa watoto wa Kike.

Akizungumza na Mtandao wa Hivi Sasa wakati wa Kongamano la kuonesha kazi zinazofanywa na CDF Mkurungenzi wa jukwaa la utu wa mtoto CDF Ndg. Koshuma Mtengeti amesema licha ya Ndoa za utotoni kuwa changamoto katika mkoa wa Tabora iko pia mikoa mingine ambayo inakumbwa na changamoto kama hizo.

“Mkoa kama Manyara bado unaongoza kwa ukeketaji, Katavi Mimba za utotoni, Singida, Dodoma na Mara bado kuna changamoto kubwa dhidi ya ukatili wa mtoto wa kike”Amesema Mtengeti.

Kwa upande wake Mkurugenzi maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Bi Margaret Mussai amesema mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto unaendelea kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Margaret Mussai Mkurugenzi Maendeleo ya Watoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Ameongeza kuwa lengo hilo litatimia kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama CDF ambao tayari wameshaanza  kutoa elimu kwa watoto wa kike ili  waweze kutimiza ndoto zao.

Kongamano hilo limewakutanisha Mabinti waliojengewa uwezo wa kujua haki zao hasa za kijamii, Mabinti waliojengewa uwezo wa kijasiriamali wengi wakiwa walioathirika na Vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni