Habari/News

Udart yaitosa Max Malipo,yaingia mkataba na TTCL

Tarehe April 14, 2018

Moja ya Mabasi ya Mwendokasi

Kampuni ya Usafirisha wa mabasi yaendayo Haraka(Udart) imeingia Mkataba na Kampuni ya Simu(TTCL) kufuatia kumaliza mkataba na kampuni ya Max Malipo Africa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa kampuni hiyo, Deus Bugaywa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko hayo amesema mabadiliko hayo ni moja ya njia ya kuboresha huduma zao ambapo TTCL kutokana na kuwa na mkongo wa taifa wanaamini wateja wao watapata huduma iliyo bora.

Akizungumzia kuhusu wafanyakazi waliokuwa wakikatisha tiketi, amesema wataendelea na ajira zao kwani hata awali walikuwa wanaripoti kwa Max Malipo lakini masuala ya mshahara walikuwa wakipewa na Udart.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni