Habari/News

Uchambuzi wa Zitto Kabwe Kusinyaa ukuaji Uchumi,Sakata la Airtel

Tarehe December 22, 2017

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amesema ukuaji wa Uchumi wa nchi ya Tanzania unasinyaa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto amesema Uchambuzi wa takwimu zilizotolewa na NBS hauwezi kuwa kosa kwa namna yeyote ile. Sera za Uchumi za Serikali ya Awamu ya zilizopelekea kuanguka kwa mikopo kwenda sekta binafsi na hivyo ugavi wa fedha ( money supply M3 ) zimesababisha ukuaji wa Uchumi wa nchi  kusinyaa.

Amesema Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF ) wamethibitisha hilo kwenye Taarifa yao na wameagiza Serikali kutazama upya vyanzo vyao vya Takwimu.

“Rais John Pombe Magufuli hawezi kuzuia uchambuzi huru wa kisera na pia takwimu za Serikali zinakosoleka na tutaendelea kutoa takwimu mbadala pale NBS wanapotoa Takwimu za uongo kufurahisha watawala.”Amesema Zitto Kabwe.

Kwa upande wa sakata la Kampuni ya Airtel Zitto amesema Serikali inaweza kuunda tume kutazama namna ubinafsishaji ulivyofanyika na kuchukua hatua za kisayansi baada ya matokeo ya kazi hiyo.

“Ni ukweli usio na shaka kuwa kampuni ya Celtel (sasa Airtel) haikulipa chochote kuwezesha kumiliki hisa kwenye Celtel Tanzania na pia uuzwaji wa Celtel kwenda Zain na kisha Airtel ulisababisha Tanzania kupoteza mapato ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax),” amesema Zitto Kabwe.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni