Habari/News

Uchaguzi Kenya: Hali ya mitaa baada ya Kenyatta kutangazwa mshindi

Tarehe August 12, 2017

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akisakata Muziki Ikulu.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akisakata Muziki Ikulu.

Maafisa wa Polisi nchini Kenya walilazimika kukabiliana na waandamanaji waliojitokeza barabarani muda mfupi baada ya Rais Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais hapo jana jioni.

Hatahivyo, hali imeripotiwa kuwa tulivu katika maeneo mengi ya miji asubuhi ya leo Jumamosi.

Maeneo yaliyoathiriwa na vurugu kati ya polisi na waandamanaji Ijumaa jioni ni Kisumu Magharibi mwa Kenya pamoja na baadhi ya mitaa Jijini Nairobi.

Katika mtaa wa mabanda wa Kibera, kelele zilisheheni hewani baada ya matokeo kutangazwa.

Katika maeneo ya Siaya, Kisumu na Migori wafuasi wa upinzani waliandamana kupinga matokeo.

Mjini Kisumu, ngome ya mgombea wa upinzani Raila Odinga, polisi walitumia helikopta kushika doria kutoka angani Ijumaa jioni.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, katika mitaa ya Buruburu na maeneo ya Kiambu, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya makundi mawili.

Kundi moja lilikuwa linasherehekea ushindi na jingine likipinga matokeo hayo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni