Habari/News

Tundu Lissu atimkia Ughaibuni

Tarehe January 6, 2018

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu leo ameondoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwenda nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Aidha, Lissu ameondoka leo  saa 2.30 asubuhi ya leo Jumamosi na Ndege ya Shirika la Kenya akiambatana na mke wake, Alicia.

Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa ni  baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma.

Mwanasiasa huyo amesindikizwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na watoto wake pacha, Augustino na Edward, ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni