Habari/News

Trump kutangaza Jerusalem Mji Mkuu wa Israel licha ya mapingamizi

Tarehe December 6, 2017

Mji wa Jerusalem.

Ikulu ya White House, Marekani imethibitisha kuwa Rais, Donald Trump leo atazungumza kuhusiana na kutangaza rasmi uamuzi wa kuhamishia ubalozi wa Marekani Mjini Jerusalem licha ya pingamizi kutoka mataifa mengine.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu hiyo, Sarah Sanders amesema kuwa Trump alizungumza na baadhi ya viongozi siku ya jumanne kuhusu mipango yake ya kuhamishia ubalozi huo kutoka Tel Aviv na kuupeleka Jerusalem.

“Amezungumza na baadhi ya viongozi asubuhi ya jana na atendelea kuwa na majadiliano na wadau wanaohusika lakini atafanya maamuzi yenye umuhimu kwa Marekani,” amesema Sanders.

Wakati huo huo viongozi wa Palestina, Misri, Jordan na Saudi Arabia, wametoa onyo kwa Rais Trump kuwa kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi za kuleta amani mashariki ya kati.

Kiongozi mkubwa wa Hamas, Khalili al Haya, amewataka wote wanaounga mkono Palestina kuungana na kupinga jitihada zozote za kuhamishia ubalozi huo Mjini Jerusalem

“Suala la Jerusalem ni suala la msingi sana, leo Hamas inawataka watu wote wanaounga mkono Palestina na kusimama pamoja juu ya suala hili, kuna jitihada zinazofanywa na Hamas nje ya Palestina, Lebanon na sehemu nyingine walipo wahamiaji,” amesema Khalili.

“Tunawataka wote kupinga mpango huu wa marekani kuhusu Jerusalem,” amesisitiza.

Mbali na kuwa Jerusalem imekuwa haitambuliki Kimataifa, Israel imekuwa ikiitambua Jerusalem kama Mji wake Mkuu huku Palestina nao imekua ikidai Jerusalem Mashariki kuwa ni Mji Mkuu wao.

Marekani itakua nchi ya kwanza kutambua Jerusalem kama Mji Mkuu tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka 1948.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni