Tarehe January 5, 2018
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari,TMA imesema mvua hiyo iliyoanza jna itanyesha pia leo ijumaa.
Mikoa ambayop itaathirika na mvua hizo ni pamoja na Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani
Taarifa hiyo imeongeza kuwa upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini; kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini, na hali ya bahari inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.
Matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5, 2018 ni kutakuwa na kuongezeka kwa mvua katika mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.
Maoni