Afya

TFDA yazifuatia usajili dawa aina 3

Tarehe November 9, 2017

Dawa zenye madhara zafutiwa usajili.

Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini, TFDA,imepiga stop matumizi ya dawa aina tatu ambazo zinadaiwa kuwa na madhara katika mwili wa mtumiaji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, wakati akifungua mafunzo ya wakufunzi wa ufuatiliaji kuhusu ufundishaji na uhamasishaji wa masuala ya udhibiti wa madhara yatokanayo na matumizi dawa amesema dawa zilizofutiwa usajili zina madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Amezitaja dawa hizo kuwa ni dawa ya sindano aina ya Chloramphenical kwenye soko baada ya Shirika la Afya Duniani, WHO, kubaini dawa hiyo ina madhara kwa watumiaji, Pia mamlaka hiyo imefuta usajili wa dawa zingine kama vile Ketoconazole, pamoja na Celecoxib baada ya kuthibitika zina madhara kwa watumiaji.

Katika mafunzo hayo TFDA imeweza kuongeza idadi ya wakufunzi  kutoka 73 hadi 133 kwa ajili ya kufundisha usalama wa dawa hapa nchini.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni