Habari/News

Takukuru yamsaka aliyekuwa mhasibu wake kwa kuwa na mali na pesa nyingi

Tarehe November 14, 2017

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo imetangaza kuwa inamsaka aliyekuwa mhasibu wake, Godfrey John Gugai, kwa kumiliki mali zisizoendana na kipato chake.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kuahidi kuwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo atazawadiwa Shilingi Milioni 10.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kujipatia mali hizo kutokana na matumizi mabaya ya ofisi, ikiwemo majumba ya kifahari mawili ya aina ya ghorofa yaliyopo Kinondoni, Nyumba za kupangisha ‘Apartments’ zilizopo Mbweni JKT na Kinondoni Jijini Dar es Salaam  na maeneo mengine ya nchi ikiwemo Mwanza.

Mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kuwa na viwanja vingi katika maeneo mbalimbali nchini katika karibu mikoa yote nchini.

Wakati huohuo, Takukuru imesema kuwa wamepokea wito wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wa kumchunguza aliyewahi kuwa waziri katika wizara hiyo na Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe. Lazaro Nyalandu na kudai kuwa kama watamkuta na hatia atafikishwa mahali panakostahili.

Waziri Kigwangalla ameitaka Takukuru kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kumchunguza Mhe. Nyalandu aliyehamia upinzani hivi karibuni akitokea CCM kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kuikosesha Serikali mapato ya Shilingi Bilioni 32 kwa miaka miwili aliyohudumu kama Waziri wa Maliasili kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni