Habari/News

Tabia ya wanaume kutembea na mabinti wadogo yamchefua Mama Samia

Tarehe December 3, 2017

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu.

Wanaume hapa nchini wametakiwa  kuacha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo, kwa kuona wakubwa wenzao hawana ladha ile wanayoitaka.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu  wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani,na kusema kwamba kitendo cha wanaume hao kuwafuata watoto wadogo licha ya kujua wameambukizwa ili tu kupata ladha yao, ni dhambi kubwa ambayo hata Mungu hawezi samehe.

Kauli hiyo  inajiri wakati maambukizi ya VVU na UKIMWI bado ni tatizo katika nchini ambapo Takriban watu 1,400,000 wanakadiriwa kuwa na VVU. Asilimia 40% ya maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa vijana wenye umiri wa miaka 15-24.

Wanaume na nyinyi muwe na maadili, wanaume wakubwa mnahisi labda wakubwa wenzenu wamechuja hawana ladha ile ambayo mngependa kuipata, kwa hiyo mnahamia kwa wototo wadogo, huu si mwendo mzuri, hawa ni watoto wetu, hili ni taifa la kesho, na wengine wanaijua kabisa kwamba wameshaambukizwa, na wakubwa wenzao wanajua wameambukizwa, wanashifti kwa watoto ambao hawawajui kwa kutumia vicent kidogo, huu ni uuaji wa makusudi na Mungu hatawasamehe” amesema Mama Samia

Aidha makundi maalum kama vile wanaojidunga madawa ya kulevya, wanaofanya biashara ya ngono na wale wanaoajamiiana kwa jinsia moja wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi.  Makundi mengine ya walio katika hatari ni waendesha magari ya masafa marefu, wavuvi na wananchi wa kwenye migodi.

Hata hivyo utafiti wa viashiria vya Malaria na UKIMWI wa mwaka 2011/12 umebaini kuwa kuna matumizi duni ya kondom, kwani ni asilimia 27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja waliokiri kutumia kondom mara ya mwisho walipofanya ngono.

Hivyo Serikali  imesema  itaendelea kununua na kusambaza kondom kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU, magonjwa ya ngono na mimba zisizo tarajiwa ikiwa ni mojawapo ya afua hizo za kudhibiti maambukizi ya VVU.

Dunia jana  imeadhimisha siku ya UKIMWI, ambapo sherehe hizo kitaifa zimefanyika jijini Dar es salaam katika viwanja vya mnazi mmoja.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni