Habari/News

Taarifa ya TMA kuhusu hali ya hewa

Tarehe April 17, 2018

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali unaozidi km 40 kwa saa katika maeneo yote ya pwani kuanzia saa 24 zijazo kutoka sasa.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya jana (Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kunatarajiwa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa.

Mikoa hiyo ni  ya Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Kigoma, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha na Manyara huku upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kusini kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni