Habari/News

Marufuku kuzungumza siasa, dini au biashara kwenye daladala na mabasi

Tarehe November 15, 2017

Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa, mahubiri ya dini na kufanya biashara wawapo safarini.

Agizo hilo limetangazwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Lingadi Ngewe na kwamba abiria, dereva au utingo atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Agizo hilo pia linahusisha kupiga nyimbo zisizo na maadili au kuonesha video ambazo hazijaruhusiwa nchini.

Bila kutaja ni sheria na kanuni ipi, Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji.

“Tutaanza kuzuia wasafiri kuacha kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara pindi abiria wawapo ndani ya basi. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi,” amesema na kuongeza

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni