Habari/News

Shinikizo la kujiuzulu laendelea kumtafuna Rais Zuma

Tarehe February 6, 2018

Rais Jacob Zuma.

Hatimaye, Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeitisha mkutano wa viongozi wake wa juu siku ya jumatano,huku kukiwa na taarifa kwamba mkutano huo ni kwaajili ya kujadili shinikizo lakumtaka rais Jacob Zuma kuachia madaraka.

Kauli ya cha cha ANC iliyotolewa kuhusiana na mkutano huo imesema kuwa,wanakutana kujadili ubadilishanaji madaraka kutoka Rais Zuma kama mwenyekiti wa zamani na sasa Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama hicho.

Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho walilazimika kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya rais Zuma.

Hadi sasa rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni