Afya

Serikali yazitaka hospitali kugawa bure dawa za Malaria

Tarehe April 24, 2018

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imevitaka   vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Zahanati ya Mwandiga iliyopo wilayani Kigoma Mkoa wa Kigoma katika akiwa anangalia hali ya matibabu dhidi ya malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya Malaria Duniani

Ameongeza kuwa  endapo mtoa huduma ataenda kinyume na hilo atachukuliwa hatua stahiki dhidi yake.

“Nawaagiza waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuweka matangazo yanayooonyesha kipimo cha haraka cha Malaria, dawa za kutibu Malaria ya mseto na sindano ya kutibu malaria kali ni bure kwenye kila zahanati, kituo cha afya na hospitali ya serikali”, amesema Waziri Ummy.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni